Tuesday, September 28, 2010

RATIBA YA MIKUTANO YA NJE WIKI HII. 2 OKTOBA NA 3 OKTOBA

Jumamosi Tarehe 2/10 mkutano utafanyika RTD-SALASALA WAZO.
Jumapili Tarehe  3/10 mkutano utafanyika MLALAKUWA-SURVEY.
Mikutano ya ndani nayo inaendelea,kama kawaida.
Ni jukumu la kila mpiganaji kutafuta Kura,kupiga kura na Kulinda kura.
WOTE MNAKARIBISHWA KUHUDHURIA,
TUSHIRIKIANE KULETA MABADILIKO.

Sunday, September 26, 2010

HALIMA MDEE ATEMA CHECHE TANKI BOVU-MBEZI BEACH

Mgombea Ubunge wa jimbo la kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mheshimwa Halima Mdee,aliendelea na mlolongo wa kampeni zake za Ubunge wa Jimbo hilo jumapili tarehe 26,kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara uliojaza umati mkubwa wa watu katika eneo la Tanki bovu,mkabala na baranbara ya Bagamoyo.
 Kama kawaida yake Mheshimiwa Mdee,aliwaeleza wakazi hao kuhusu matokeo ya Ufisadi katika manispaa ya Kinondoni na jinsi alivyojitoa muhanga kupambana nayo na kwa ajili ya mustakabali wa wakazi wa jimbo la kawe,hususani kata ya mbezi juu.
 Kamanda Halima Mdee ataendelea na kampeni zake katika mbio za ubunge katikati ya wiki kwa kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote kumi na moja za jimbo la Kawe.

Kamnda Halima Mdee akimtambulisha mama yake mzazi kwa wapiga kura wake.

Shughuri zote zilisimama kwa muda,ili kumsikiliza mpiganaji na mkombozi wa wakazi wa Kawe,Mh Halima mdee.

Wapiga Kura wakifuatilia kwa karibu mkutano huu,hii ni sehemu tu ya mwamko wa wakazi wa Mbezi juu na tanki bovu.

Wake kwa waume 2010,Hakuna kulala mpaka kieleweke!

KAMANDA WA CHADEMA ALIEPANIA KULETA MABADILIKO KAWE

 Halima James Mdee
alizaliwa Machi 18, 1978 katika Kijiji cha Makanya, Wilaya ya Moshi Vijijini, ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa James Mdee ambaye alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya chekechekea.
Alianza kusoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1991. Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki mwaka 1992 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995.