Sunday, September 26, 2010

KAMANDA WA CHADEMA ALIEPANIA KULETA MABADILIKO KAWE

 Halima James Mdee
alizaliwa Machi 18, 1978 katika Kijiji cha Makanya, Wilaya ya Moshi Vijijini, ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa James Mdee ambaye alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya chekechekea.
Alianza kusoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1991. Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki mwaka 1992 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995.
{Pichani Kamanda Halima Mdee akichukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la kawe}
Mwaka 1996 hadi 1998 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro na 1999 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea sheria na kuhitimu mwaka 2003.
Aliajiriwa na Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana mwaka 2004 akiwa Ofisa Maendeleo kama mwanasheria mpaka mwaka 2005 alipoamua kuacha kazi na kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu, ambako alishiriki kuwapigia kampeni wagombea wa CHADEMA kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.
Mdee alizaliwa katika familia ya Wakristo na alibatizwa na kuitwa Theodosia, hata hivyo anatumia zaidi jina alilorithi kutoka kwa bibi yake mzaa baba, Halima.
Ukoo wake ni waumini wa dini ya Kiislamu isipokuwa baba yake na kaka yake ambao walibatizwa na familia yao ikaridhia wawe Wakatoliki kama shukurani kwa kanisa kutokana na msaada mkubwa lilitoa kwa familia hiyo ambao Mdee alikataa kuueleza.
Mbali na ubunge, pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la CHADEMA, na ofisa katika kurugenzi ya sheria.

10 comments:

  1. we ni shujaa wa ukweli dada.... keep it up.

    ReplyDelete
  2. Safi sana, nimefurahi kuona mwanamke shujaa kama wewe. songa mbele.

    ReplyDelete
  3. Je umeanzisha akaunti ya watu kuweza kuchangia kampeni zako?Ingekuwa vizuri ukaiweka mbagani(hadharani) ili kama kuna watu wanaoweza kukuchangia wafanye hivyo. Asante

    ReplyDelete
  4. Halima nakutakia kila la kheri! 2010 hatutaki viongozi vijana tu bali twataka "Vijana makini"! Mapinduzi daima!!

    ReplyDelete
  5. People's power ... Halima u have my vote maana nakufahamu kiutendaji katika bunge letu. Kama chama mara nyingi wamekuwa wakikukalisha pale unapochangia kwenye hoja tete kwa sababu ya hoja nzito...

    ReplyDelete
  6. Halima, Nakukubali dada yangu, kwa kweli kutokana na msimamo wako, naamini kwa mshikamano pamoja na makamanda wenzio,mnaweza kutuvusha kututoa hapa tulipokwama kutufikisha katika bandari ya salama, tunakotarajia kuanza maisha ya Tanzania yetu mpya!

    ReplyDelete
  7. Halima kaza buti, tunahitaji kina dada ngangali kama wewe, tumechoshwa na umaarufu wa jina lakini vitendo vinakuwa hafifu, hivo tukomboe vijana wenzako na ufisadi uliokithili.Mungu akulinde na akupe nguvu kuyatekeleza yote yaliyo kwenye ilani yenu, tunakuombea siku zote.
    Isaac Mwaipopo

    ReplyDelete
  8. Viongozi wengi wamekaa madarakani karne na karne na kuwa na majina maarufu ila umaarufu wao ungekuwa unatenda kazi, basi tungekuwa mbali na mabomba yangekuwa yanatoa maziwa kama sio asali, hivo mwaka huu nawashauri watanzania wenzangu kumchagua mtu makini au watu makini kwa ujumla pamoja na Dada Halima Mdee, kwani ameonesha uwezo akiwa bungeni ikiwa ni pamoja na kupinga ufisadi wa ardhi kinondoni. Mungu akupe afya na akulinde dhidi ya maadui zako ambao pia ni maadui zetu wakubwa ambao ni mafisadi. Kaza buti dada.

    ReplyDelete
  9. Mdogo wangu Theodosia Halima James Mdee. Nakutakia kila la kheri katika jitihada zako. Ushauri wangu kuwa na hofu ya Mungu na Mtegemee Mungu utafika mbali. I do not know if you are married if yet please find a caring and loving husband. Avoid abusive men they can distort your potentials. lastly, upinzani wa kweli ni ule unaoleta transformation kwa kukosoa mifumo kandamizi yote, majukwaani, kwenye vikao na mikutano, mafunzo na hata kufungua kesi za msingi kama zile za kukosoa mifumo kandamizi kama mtu kugombea wakati akiwa rais. kuwa na tume iliyowekwa na chama tawala, chama tawala kumiliki mali na rasilimali zilizokuwa zinamilikiwa na kuchangiwa na wananchi wote wa Tanzania kabla ya vyama vingi n.k.

    ReplyDelete
  10. Tunaomba aanzishe blog yake tuwe tunampa ripoti, hasa kuhusu matatizo ya maji, umeme, elimu, afya, huduma za jamii na miundo mbinu jimboni kawe. hasa bunju b.

    ReplyDelete