Friday, October 1, 2010

MDEE APASUA JIPU,TEGETA-WAZO!........

Alhamisi ya tarehe 30 mwez 9,mgombea ubunge kwa tiketi ya chadema jimbo la kawe Mh Halima James Mdee,alipasua jipu lingine juu ya ufisadi uliokithiri katika manispaa ya kinondoni.Akiwahutubia wapiga kura wa eneo la Kwa Panga,Tegeta Wazo hill,.Mh Mdee aliwaeleza wananchi juu ya Kupuuzwa kwa madai ya wanakijiji wa kijiji caha CHASIMBA juu ya mgogoro wao wa Ardhi ambao aliusimamia wakati akiwa Mbunge wa viti maalumu.Mheshimiwa Mdee ataendelea na mikutano mingine wikiend hii katika maeneo ya Salasala na Mlalakuwa survey.




2 comments:

  1. Dada Halima
    Nimeweka bango lako la kuomba mchango katika Jamii Forum ambako watu wengi wanataka kukuchangia lakini wengine wanasema ungeanzisha njia ya simu au nyingine nyepesi ambayo mtu anaweza kukuchangia. Pindi ukiiweka basi nijuze ili niwajuze. Vilevile ingekuwa vizuri kama ungeweze kutoa habari zako katika Jamii Forum pamoja na vipande vya video vya mikutano yako. Nami nitatuma mchango wangu mdogo katika akaunti yako. Mapambano yanaendelea...
    Rugemeleza Nshala

    ReplyDelete
  2. Tunaomba aanzishe blog yake tuwe tunampa ripoti, hasa kuhusu matatizo ya maji, umeme, elimu, afya, huduma za jamii na miundo mbinu huku kawe, mbezi beach, goba, salasala, kunduchi, tegeta, boko, bunju a na b.

    Bunju B

    ReplyDelete